Photo of the Remarkables mountain range in Queenstown, New Zealand.
Photo of the Remarkables mountain range in Queenstown, New Zealand.

Tuesday, September 5, 2017

5 September 2017, Spika Ndugai:Wabunge wanatakiwa kusoma katiba za vyama vyao

Mkutano wa nane wa Bunge la kumi na moja umeanza hii leo mjini Dodoma ambapo pamoja na shughuli nyingine wabunge saba kutoka chama cha wananchi - CUF wamekula kiapo.
Akizungumza baada ya kumaliza kuwaapisha wabunge saba wa chama cha CUF , Spika wa bunge Job Ndugai amewataka wabunge wote kusoma katiba za vyama vyao na kuziheshimu kwa kuwa uhusiano wa wabunge na Vyama vyao vya Siasa una uzito wa pekee.
Katika hatua nyingine bunge limeendelea na maswali na majibu ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki amesema wakati wowote kuanzia sasa watumishi wa umma watapandishwa mishahara na madaraja.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Tamisemi, George Simbachawene amesema wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wanafanya mpango wa kuzirudishia hadhi shule kongwe zilizokuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita.
Baada ya Kipindi cha maswali na majibu hii leo miswada miwili itawasilishwa.


No comments:

Post a Comment

Photo of the Remarkables mountain range in Queenstown, New Zealand.