Pwani. Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara,
Charles Mwijage, kuwanyang’anya viwanda wamiliki ambao wameshindwa
kuviendeleza.
Ameyazungumza hayo leo (Alhamisi) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.
“Kipindi cha nyuma tulipofanya makosa ni pale tulipouza viwanda kwa watu
binafsi, sasa kuna viwanda 197 vimeshakufa waliouziwa
hawajishughulishi na vingine vipo kama magofu,” amesema.
Kutokana na hilo, Rais amesema; "natoa wito kwa wote waliouziwa viwanda
kipindi cha nyuma na sasa wameshindwa kuviendeleza , naagiza sasa basi
mrudishe na wewe Waziri Mwijage tumia hata nguvu kama kuwaweka ndani
weka tu siku akitoka huko atakuta kiwanda kimeanza kazi."
No comments:
Post a Comment